DODOMA: Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, imebaini Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), ilitoa zabuni ya vifaa vya maabara vya upimaji wa Covid 19 bila ya kufuata ushauri wa wataalam na kubaini kuwa kampuni iliyopewa zabuni hiyo haikuwa mtengenezaji wa vifaa hivyo, kinyume na masharti ya zabuni.
CAG Kichere amesema baada ya vifaa hivyo kufika, MSD ilibaini kuwa vifaa hivyo havifai kwa mashine zetu, hata hivyo MSD ililipa fedha zote.
Kichere amesema mapendekezo ni wafanyakazi waliohusika kurudisha fedha hizo za umma.