CAG abaini mikopo ya Sh Bil 88 haikukusanywa

MAMLAKA za Serikali za Mitaa hazikuweza kukusanya mikopo iliyotolewa kwenye vikundi vya Wanawake, Vijana, na Watu wenye Ulemavu, yenye jumla ya shilingi bilioni 88.42

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG ), CPA Charles Kichere, imebaini hali hiyo imetokana na kutokuwa na ujuzi wa kutosha kwenye Idara za Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa kufanya upembuzi yakinifu kwa vikundi vilivyoomba mikopo, kuvisimamia vikundi hivyo, kufuatilia urejeshaji wa mikopo, na kutoa mafunzo ya biashara kwa wanufaika.

Ripoti hiyo imeoneysha kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 2.25 zinahusiana na vikundi vilivyoacha shughuli za biashara hivyo kuleta mashaka juu ya urejeshwaji wa mikopo hiyo.

Advertisement

Pia, imebaini kuwa Mamlaka tatu za Serikali za Mitaa zilitoa shilingi milioni 895.94 kwa vikundi 48 ambavyo havikuwepo.

/* */