Card B hajarudiana na Offset

MSANII wa ‘Hip Hop’ nchini Marekani Belcalis Cephus ‘Card B’ amekanusha taarifa za kurudiana na aliyekuwa mume wake, Kiari Cephus ‘Offset’.

Cardi B ameandika kanusho hilo baada ya taarifa kuwa wamerudiana kufuatia wawili hao kuonekana wakisherehekea sikukuu ya Krismasi na watoto wao wawili Kulture na Wave.

Disemba 11, 2023 kupitia ‘Instagram live’ Cardi B alitangaza kuachana na ‘mwanahiphop’ huyo huku baadhi ya mitandao nchini Marekani iliripoti kuwa chanzo ni Offset kuwa na mwanamke mwingine.

“Najua leo imekuwa siku ya matukio sana, sifikirii kuhusu hayo, linapokuja suala la tukio la leo, sifikirii kama ni kweli, nimekuwa mwenyewe kwa muda sasa.

”aliandika Card B kwenye mtandao X wakati akijibu maoni ya baadhi ya wadau.

Habari Zifananazo

Back to top button