Card B, Offset wamerudiana?
LICHA ya taarifa za kuachana kwao hivi karibuni, wasanii Cardi B na Offset wameonekana pamoja tena na watoto wao wakisherehekea Krismasi.
Wasanii hao walichapisha video kwenye kurasa zao za Instagram wakifurahi na watoto wao, Kulture wa miaka 5 na Wave wa miaka 2 pamoja na watoto wengine.
Kuonekana kwao pamoja unakuja baada ya hivi karibuni Cardi kutangaza kutengana na Offset baada ya takriban miaka sita ya ndoa.
Kabla ya hapo, wawili hao waliacha kufuatana ‘Unfollow’ kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii huku kukiwa na uvumi kwamba Offset alimdanganya Cardi Kwa