Casemiro, Shaw nje, Eriksen ndani

LIGI Kuu England inaendelea leo kwa mchezo wa mapema kati ya Manchester United dhidi ya Everton mchezo utakaopigwa Uwanja wa Old Trafford saa 8:30 mchana.

Kuelekea mchezo huo, kiungo Christian Eriksen atarejea kwa mara ya kwanza tangu Januari alipoumia kifundo cha mguu. Lakini itaendelea kumkosa Carlos Casemiro aliyefungiwa michezo minne kwa kadi nyekundi dhidi ya Soton wiki tatu zilizopita.

Pia itamkosa Luke Shaw ambaye ana maumivu kwenye nyama za paja. Manchester United wamepoteza mechi moja tu kati ya 23 zilizopita za Ligi Kuu ya Uingereza (W15, D7), na kufungwa 2-1 na Brighton mwezi Agosti.

Everton wamevuna pointi 12 kutokana na michezo yao tisa ya Ligi Kuu chini ya Sean Dyche, baada ya kufikisha pointi tano pekee kati ya tisa za mwisho chini ya Frank Lampard.

Hata hivyo, wameshinda mechi mbili pekee kati ya 31 zilizopita za ugenini za ligi (D9, L20), wakishinda dhidi ya Southampton mwezi Oktoba.

Michezo mingine itakayopigwa leo ni Aston Villa dhidi ya Notts, Brentford dhidi ya Newcastle, Fulham na West Ham, Leicester na Bournemouth, Spurs dhidi ya Brighton, Wolves na Chelsea michezo yote itapigwa saa 11:00 jioni.

Mchezo wa mwisho utakuwa kati ya Soton dhidi ya Man City utapigwa saa 1:30 usiku.

Habari Zifananazo

Back to top button