CBT yazindua vifaa Korosho Marathon

 KATIKA kueleke msimu wa pili wa mbio za Korosho Marathon, Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) imezindua rasmi vifaa vitakavyotumika  katika mbio hizo zitazofanyika Septemba 2, 2023 katika viwanja vya Nangwanda Sijaona mkoani humo.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Francis Alfred amesema kuwa tayari wameshakamilisha taratibu zote za maandalizi kulekea mbio hizo ikiwemo vifaa vitavyotumika  kama vile Tshrt, medali na mifuko rasmi kwa ajili ya wakimbiaji.

Aidha, mbio hizo zitakuwa umbali wa kilomita 21 ambayo mshindi wa kwanza atapatiwa Sh milioni 4, wa mwisho katika mbio hizo Sh 400,000 pia kilomita 10 ambayo mshindi wa kwanza atapatiwa Sh milioni 2.5 wa mwisho Sh 50,000 mbio nyingine ni kilomita 5 ambayo washindi wataangaliwa taratibu zingine.

Idadi ya washiriki katika mbio hizo inakadiriwa kuwa zaidi ya 1,500 hivyo wadau na wapenda michezo nchini wametakiwa kuendelea kukamilisha taratibu za kujisajili ili kuweza kushiriki mbio hizo ambapo gharama za usajili huo ni Sh 30,000.

“Zikiwa zimebaki siku nne kuelekea korosho marathon niowaombe watanzania, wadau wa michezo na wapenda maendeleo kuendelea na taratibu za usajili ili kushiriki mbio hizo”.amesema Alfred

Habari Zifananazo

Back to top button