CCM Bagamoyo yaonya viongozi wazembe

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kimewaonya baadhi viongozi waserikali na chama kuacha tabia ya kufanyakazi kwa mazoea na badala yake wametakiwa kuwa wadilifu na waaminifu katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Hayo yalibainishwa na mwenyekiti wa chama hicho, Wilaya ya Bagamoyo, Abdusharifu Zahoro wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo, katika mbio za bendera katika kata ya Mapinga na Kerege mkoani hapa.

Amesema baadhi ya viongozi wa serikali na chama wamekuwa wakifanyakazi kwa mazoea na kushindwa kutimiza wajibu wao katika kuwatumikia wananchi na kushindwa kusimamia vema miradi ya maendeleo.

“Natoa maelekezo hasa Kwa viongozi wa Chama, mmepata nafasi mnashindwa kuwajibika na mnakaa tu pasina kazi ya kufanya, Chama hicho sio mali ya mtu binafsi lazima ifike mahala kuwajibike Kwa uaminifu na uadilifu unaopaswa katika kusimamia miradi ya maendeleo”amesema

Amesema serikali imetoa zaidi ya bilioni Mbili katika kata hizo kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo Afya,elimu na Barabara na kwamba fedha hizo zinapaswa kusimamia vema ili zifanyekazi zilizokusudiwa ya kutatua changamoto za wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha mapinduzi Wilaya ya Bagamoyo, Abubakari Mlawa amewataka viongozi wa matawi na kata kuwa uwajibikaji kwa wananchi ili wazidi kuaminika katika utendaji wao.

Mlawa amesea kuwa kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakidai kuwa viongozi wengi wa Chama na Serikali wamekuwa wakifanya maamuzi bila kuwashilikisha wananchi jambo ambalo halitakiwi.

Naye Diwani wa kata ya Kerege Said Ngatipula, alisema serikali ya awamu ya sita imetoa zaidi ya shingi Milioni 800 ambazo zimefanikiaha ujenzi wa kituo cha afya cha kata hiyo, ujenzi wa madarasa katika shule za msingi na sekondara pamoja na kutengeneza baadhi ya miundombinu ya barabara na maji.

Mbio za bendera zinaendelea katika kata zote kwa lengo la kukagua uhai wa chama, kuzindua mashina ya chama, utekelezaji wa ilani na ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x