CCM Dar wataka umoja, makundi sasa basi

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu amesema hataki makundi, rushwa wala kukatana kwenye Mkoa wa Dar es Salama na kuwataka wanachama wote wa chama hicho wavunje makundi yao.

Mtevu ameyasema hayo leo Desemba Mosi, 2022 akikabidhiwa ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam.

Mtevu alishinda kwa kura 444 katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni na kumwangusha Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Mama Kate Kamba aliyepata kura 160.

Mtevu amesema kazi yake ya kwanza ni kurudisha mshikamano, kurudisha matumaini kwa watu ambao wanasema wao  wabaya.

“Kuna watu ilikuwa wanasema wakina Mtevu wabaya, tunataka kuwaonyesha kuwa sisi sio wabaya, tunachotaka ni umoja na mshikamano, Dar es Salaam imezidi kwa migogoro, sitapenda kuona mnagombana.

“Uchaguzi umeisha makundi mvunje, sisi sote ni kitu kimoja, haina maana kugombana, na watakaoendeleza migogoro tutafungia, na msikimbilie msituni tukae humu humu kama kuonyana tuonyane.

“Na watakaobainika kula rushwa tutawafungia, tunataka Dar iliyo safi, na nikikufungia mimi hakuna wa kukufungulia.”Amesema

Aidha, Mtevu amesema hakutarajia kushinda kwa kura za kishindo na kuwashukuru wanachama wa CCM Dar es Salaam kwa kumchagua.

“Nimepata kura 440 nilijua nitashinda, lakini sikujua kama nitashinda kwa kishindo, nilijua nitashinda kutokana na timu nilizokuwa napambana nazo nilijua nitashinda ila si kwa mabao mengi hivi…; “Kila ninavyokaa nafikiria  nitaifanyia nini CCM Dar es Salaam .”

Kwa upande wa Mwenyekiti Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Khadija Ally amewashukuru wajumbe kwa kumuamini na kumpa kura za ndio.

Khadija ameaidi pia ushirikiano kwa wanachama na viongozi wote wa mkoa wa Dar es Salaam katika kutekeleza ilani ya CCM.

Amesema katika chaguzi makundi hayaepukiki ila baadaye yanakwisha baada ya uchaguzi kumalizika na kuwa wamoja kukijenga na kukiimarisha Chama.

Amesema jukumu lao kubwa kama viongozi waliochaguliwa ni kuyaunganisha makundi yote, ukizingatia kuwa chaguzi hizo ni za ndani ya chama huwa wanajipanga na siyo kushindana na kwamba umoja, mshikamano miongoni mwa wanachama ndio nguzo imara

Habari Zifananazo

Back to top button