CCM Geita wataka weledi usimamizi wa miradi

CCM Geita wataka weledi usimamizi wa miradi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Geita, kimeutaka uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kuimarisha usimamizi wa miradi inayojengwa kwa mfumo wa ‘force  Account’ ili ikamilike kwa kiwango.

Mwenyekiti wa CCM wilayani Geita, Barnabas Mapande ametoa maelekezo hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita.

Amesema mbali na serikali ya CCM kuruhusu miradi kutekelezwa kwa ‘force account’, ili mafundi wazawa wapate ajira na kunufaika moja kwa moja na miradi hiyo, lakini ni vyema usimamizi wa miradi uimarike.

Advertisement

“Wilaya yetu ya Geita, tumekuwa ni miongoni mwa wilaya chache sana, ambazo zinapatiwa fedha nyingi kutoka kwenye serikali kuu, na ukitazama hata kwenye madarasa tuliletewa fedha nyingi sana.

“Kwa hiyo fedha hizi zinapokuja kwetu, wasimamizi waweze kufuatilia, kupitia mafundi wetu wa ndani, ambao tunawaajiri kule, ili waweze kujenga kwa kiwango cha serikali, ” amesema.