CCM Mpanda wawekana sawa usajili wa kielektroniki

MAOFISA wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia weledi katika kusajili wanachama kwa mfumo wa kielektroniki.

Wito huo umetolewa na Katibu wa CCM, Wilaya ya Mpanda Sadick Kadulo, katika ufunguzi wa mafunzo maalum ya maofisa Tehema yaliyofanyika ukumbi wa CCM Wilaya.

Amesema kazi ya kusajili wanachama kwa njia ya kielektroniki ni agizo la Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, ambalo lilianza kutekelezwa mwaka 2018 na mpaka sasa Wilaya ya Mpanda ina wanachama 72,000, ambapo wanachama 22,000 tayari wamesajiliwa katika mfumo huo.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda, Method Mtepa amesema kwa sasa uchaguzi umekwisha, hivyo hakuna haja ya kuwa na mvutano ndani ya chama.

“Kusiwe na mvutano hauna haki, mvutano hauna faida, mvutano hauna sheria, uchaguzi umekwisha wote tumebaki wana CCM, wote tumebaki wanachama wa Chama cha Mapinduzi,”amesema Mtepa.

Kwa upande wake Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Taifa, Gilbert Sampa, ambaye alikua mgeni rasmi katika uzinduzi huo, amesema mtaji wa chama hicho ni kuhakikisha wanaongeza idadi ya wanachama.

 

Habari Zifananazo

Back to top button