CCM Pwani yataka umoja

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani, wameonywa kuacha tabia ya kujengeana chuki na fitna na badala yake wametakiwa kushirikiana katika maandalizi ya uchaguzi ujao wa serikali za mitaa 2024.

Mjumbe Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani, Alhaji Musa Mansour aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kata ya Kongowe, wilayani Kibaha ambapo pia alikabidhi msaada wa fedha Sh milioni 6 za ununuzi wa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi.

Alisema uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka 2024 upo karibu na kwamba wananchama hao hawapaswi kujengeana chuki, fitina, majungu na kutengeneza makundi.

“Uchaguzi upo karibu sio wakati wa kuleteana chuki, majungu na fitina tuungane na tushirikiane katika kukijenga Chama chetu ili uchaguzi ujao wa serikali za mitaa tuibuke washindi”alisema

Alikabidhi msaada huo, Mansour alisema wanaccm wanapaswa kuwakataa baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakiwagawa na kwamba ujenzi wa chama unapaswa kutekelezwa na wachama wenyewe Kwa kujitoa Kwa hali na Mali.

“Leo nimekabidhi milioni sita za ununuzi wa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi yetu ya kata lakini pia nitatoa tofali 2000 pamoja na saruji ili ujenzi uanze mara moja, Chama kinapaswa kujengwa na sisi wenyewe ..hivyo nitoe wito wengine wenye uwezo wajitokeze kujenga chama chetu”alisema

Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo, Simon Mbelwa alisema tatizo walilokuwa nalo ni ukosefu wa ofisi za chama jambo ambalo limekuwa likisababisha usumbufu wa kuendesha shughuli mbalimbali za chama na wanashukuri kwa msaada huo ambao utatua tatizo hilo.

Katibu wa CCM wa kata hiyo, Said Mbwebwe, alimshukuru Mansour Kwa msaada huo ambapo aliwataka wadau wengine wenye uwezo kuona umuhimu wa kutoa misaada mbalimbali inayo hitajika katika jamii, Chama na hata serikali.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
John Pombe Joseph Magufuli[
John Pombe Joseph Magufuli[
1 month ago

David Robert Joseph Beckham

Tangazo.PNG
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x