CCM Simiyu watakiwa kuvunja makundi

CCM Simiyu watakiwa kuvunja makundi

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa ngazi ya wilaya, wameombwa kuachana na makundi waliyokuwa nayo, wakati wakiwania nafasi walizopata, bali waanze kutekeleza majukumu yao kwa kufuata ilani ya CCM.

Ombi hilo limetolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mohamed Ally, mara baada ya kumalizika kwa chaguzi za kuwapata viongozi wa chama hicho katika ngazi za wilaya.

Alisema kuwa makundi hayaepukiki katika chaguzi zozote, ila baadaye yanakwisha baada ya uchaguzi kumalizika na kuwa wamoja kukijenga na kukiimarisha Chama.

Advertisement

Alisema ni vizuri kwa viongozi waliochaguliwa kuyaunganisha makundi yote, ukizingatia kuwa chaguzi hizo ni za ndani ya chama huwa wanajipanga na siyo kushindana.

“Wito wangu kwa ninyi Viongozi mliopata nafasi mbalimbali za uteuzi, muachane na makundi, ambayo lengo lake sio kukuza chama, bali yatawatumia katika kukidhoofisha, hivyo tekelezeni majukumu yenu kwa kuzingatia ilani ya chama, na kwa kufuata maelekezo ya Mwenyekiti wetu, Rais Samia Suluhu Hassan,” alisema.

/* */