CCM: Tanesco mjitafakari

DAR ES SALAAM: CHAMA cha Mapinduzi CCM kimelitaka Shirika la Umeme nchini TANESCO lijitafakari kwakuwa si kila sababu za TANESCO kuhusu kukatika kwa umeme nchini zina mashiko ila nyingine ni uzembe.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema chama hicho hakifurahii katika katika ya umeme hivyo kupelekea uvunjifu wa bodi ya utendaji ya TANESCO mara kadhaa.

“Ukiona Rais anavunja bodi, ujue amefikia kusema hii haivumiliki,” amesema katibu huyo.

“Je, mnaona mnafaa kumuwakilisha Dk. Samia?.” Ameuliza Makonda.

Aidha, Makonda ameitaka TANESCO kuhakikisha ahadi yake ya kuwasha kinu cha kufua umeme katika Bwawa la Nyerere JNHPP mnamo Januari, 2024 ili kupunguza makali ya umeme nchini.

Una maoni usisite kutuandikia

Je umejisajili #MwangwiwaUkarimu #EchoesofKindness
#HabarileoUPDATES

Habari Zifananazo

Back to top button