CCM, Tanga yawataka watendaji kumaliza kero za Wananchi

TANGA: Chama Cha mapinduzi mkoani Tanga kimewataka watendaji kuacha kukaa ofisi bali watoke kwenda kutatua kero za wananchi Ili kuharakisha upatikanaji wa maendeleo kwenye maeneo yao.

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurahman wakati akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Gawani kilichopo katika kata ya Kigombe wilayani Muheza.

Amesema kuwa serikali inajitahidi kuleta miradi mingi ya maendeleo Ili kusaidia kutatua changamoto zilizopo lakini tatizo lipo Kwa watendaji ambao wanakaa tuu ofisini badala ya kushuka kwenda Kwa wananchi.

“Niwaagize watendaji mkoani hapa tokeni maofisini muwafuate Wananchi mkawatatulie kero zao badala ya kuwasubiri waje maofisini kwenu kwakufanya hivyo mnakwamisha maendeleo”amesema Mwenyekiti Rajab.

Nae Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma amesema kuwa Ili kumaliza changamoto ya uhaba wa maji iliyodumu kwa muda mrefu katika kata hiyo wamepatiwa mradi wenye thamani ya Sh Bilioni 1.3.

“Ndani ya kipindi kifupi changamoto ya uhaba wa maji safi na salama katika kata hii inakwenda kwisha baada ya mradi huo kukamilika “amesema Mbunge huyo

 

Habari Zifananazo

Back to top button