CCM wamtega Mbowe

DAR ES SALAAM; Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM,  Amos Makalla,  ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, amesema wamesikia kauli ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, hivyo ajiandae kuitekeleza.

Akizungumza leo ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Makalla amesema amemskia Mbowe, akisema lazima wachukue ushindi wa majimbo ya Kaskazini yote na akishindwa atajiuzulu.

“Sasa nasi tumuambie na tumemrekodi kuwa ajiandae kutoka mana sisi tutachukua majimbo yote ya Kaskazini na Tanzania yote, sisi sio wabaguzi tunapiga kote sio yeye anabagua, najua anajiandaa na uenyeketi.

“Niwaambie vyama vya upinzani vimekosa mvuto na muelekeo na ndio Maana watu wao wanazidi kuja kwetu Chama cha Mapinduzi na hapa kuna Diwani wa Chadema atakakuja nimpokee na bado tutapiga bomu lingine mpaka wakimbiane,” amesema Makalla.

Habari Zifananazo

Back to top button