CCM yachukizwa na udhalilishaji wa Heche

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani vikali kitendo cha Mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuonekana katika video katika Mitandao ya kijamii akimnyima fursa ya kufanya kazi mwananchi moja kwa sababu alikuwa amevaa fulana ya CCM na kusema tukio hilo ni kuvuja katiba ya nchi.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma ambapo amesema tukio hilo licha ya kuvunja katiba linarudisha nyuma juhudi za Rais Samia na viongozi wa vyama vya siasa katika kuleta maridhiano na kusema vyombo vya Dola vinapaswa kumshughulikia.

Kauli ya Shaka imekuja baada ya ‘video clip’ baada ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyomuhusisha mwanachama wa Chadema Mwalimu Chacha Heche kaka wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema John Heche dhidi ya mzee mmoja mkoani Mara.

Video hiyo inamuonyesha Chacha akimlazimisha mzee huyo kuvua fulana yenye nembo ya CCM aliyoivaa kwa mapenzi yake binafsi.

“Kijana huyo ameonekana akimtweza na kumlazimisha kuvua fulana hiyo ya CCM ili kuweza kumpa ajira mzee huyo na asipofanya hivyo basi angemfukuza, kitendo hicho ni ukiukwajji wa haki za binadamu na uhuru wa mtanzania kuamini katika itikadi aitakayo ya chama cha siasa kwa mjuibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 3 (1) na Ibara ya 20 (1) na sheria namba 5 ya vyama vya siasa na marekebisho yake ya mwaka 2018.”Amesema Shaka

Habari Zifananazo

Back to top button