CCM yakemea rushwa Muleba

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Paul Makonda amekemea vitendo vya rushwa vilivyopo Wilaya ya Muleba mkoani Kagera huku akiahidi kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kukomesha vitendo hivyo.

Amesema miongoni mwa maeneo yenye harufu ya rushwa ni kwenye maneno ya vitalu, ofisi za watumishi wa Umma na kwenye vituo vya polisi.

Makonda alisema hayo Novemba 9, 2023 aliposimama kuzungumza na wananchi wa wilaya hiyo waliosisima barabara kusubiri msafara wake ili kuongea ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya Kanda ya Ziwa.

“Tutaongeza na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru na tutaleta timu ili kuhakikisha rushwa si sehemu ya wilaya ya Muleba,” amesema Makonda

Kuhusu changamoto ya maji katika wilaya hiyo kiongozi huyo alisema atazungumza na Waziri wa Maji, Juma Aweso ili kuona mipango ya wizara hiyo ya kumaliza changamoto ya maji katika wilaya hiyo.

“kutokana na mazingira yalivyo kabla sijaondoka chato nitaongea na Waziri wa Maji ili aniambie mpango wao ni upi wa kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Muleba wanapata maji,” alisema.

Pia aliwataka viongozi wa CCM Wilaya ya Muleba wahakikishe ofisi ya chama hicho zinakamilaka pamoja na wahakikishe wanaeleza taarifa za mapato za chama katika wilaya hiyo.

Aliwasihi wakazi wa Muleba kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi ambazo ameendelea kufanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi ndio maana fedha zinazotelewa anataka zisimamiwe vizuri ili kukamilisha ilani ya CCM.

“Rais Samia Suluhu Hassan nataka ukiona kila kitu kinaenda vizuri na mkiona Kuna sehemu hapajaenda sawa si dhamira yake ni sisi wasaidizi wake tumeshindwa kutimiza dhamira yake,” alisema Makonda.

Habari Zifananazo

Back to top button