CCM yaongeza viti Wajumbe Halmashauri Kuu

Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Samia Suluhu amesema ili kupanua wigo, halmashauri kuu ya chama hicho leo imeamua kuwasilisha mapendekezo ya kuongeza nafasi za Wajumbe wa Halmashauri Kuu kutoka viti 15 kwa Bara na viti 15 kwa Zanzibar na kuwa na viti 20 Bara na 20 Zanzibar.

#SamiaMwenyekiti#

Rais Dk Samia ametoa uamuzi huo umetolewa katika Mkutano Mkuu wa 10 wa chama hicho, huku Rais Samia akisisitiza kuwa matarajio yake kuwa wajumbe wa mkutano huo watambue dhamira njema ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa kuhusu mapendekezo ya kuongeza idadi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ili kukipa chama sura mpya kwa utekelezaji bora wa mipango yake.

“Wote walioteuliwa kugombea nafasi walizoomba ni washindi kwasababu Chama kimewaamini kuwa yeyote ambaye atachaguliwa huko nyuma na leo ni mwanachama ambaye anaweza kuongeza nguvu zake katika kukijenga chama,” amesema Dk Samia.

Dk Samia ametoa wito kwa wanachama walioteuliwa kugombea nafasi za ujumbe wa halmashauri kuu kutambua lengo la uchaguzi si kutafuta ushindi wa mtu mmoja mmoja bali ni mkakati wa kujiimarisha ili kutafuta ushindi wa chama katika chaguzi zijazo.

Viongozi mbalimbali wakiingia kwenye Mkutano wa 10 wa Chama Cha Mapinduzi

 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Abdulrahman Kinana akisalimia na baadhi ya viongozi wa CCM

 

Habari Zifananazo

Back to top button