CCM yashinda kata zote sita Udiwani

MBEYA,Mbarali: Chama cha Mapinduzi (CCM), licha ya kushinda Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Mbarali kwa mgombea wake Bahati Ndingo kupata kura 44,334 kati ya kura 56,095 halali zilizopigwa, pia chama hicho kimeshinda kata zote sita katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi wa kata zilizofanya uchaguzi yanaonesha kuwa Helman Masila wa CCM ameshinda kwenye Kata ya Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Kayombo Christopher Fabian ameshinda kwenye Kata ya Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Matokeo mengine yanaonesha kuwa Ng’wanza Venance Mathias ameshinda kwenye Kata ya Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Peter Dastan Massawe wa CCM ameshinda katika Kata ya Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Simon Rogath Massawe wa CCM ameshinda katika Kata ya Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Diwani Twaibu Ngonyani wa CCM ameshinda katika Kata ya Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.

 

 

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x