CCM yatoa neno wanaotaka ubunge

DAR ES SALAAM: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wanachama wa chama hicho kuacha kufikiria nafasi za udiwani, ubunge kwa sasa badala yake wawaunge mkono waliopo katika nafasi hizo.

Hayo yameelezwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda katika mkutano wake na waandishi wa habari kutoa tathmini ya robo mwaka ya utendaji kazi wa chama hicho, katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, jijini Dar es Salaam.

“Chokochoko zote zinazofanywa ziachwe, waacheni wabunge wafanye kazi,” amesema Katibu huyo.

Amesema CCM inawatambua viongozi waliopo na inawaunga mkono, hivyo imewataka wanachama wake kuacha kuwapa presha viongozi waliopo kwani wakati muafaka ukifika watawania nafasi hizo.

Una maoni usisite kutuandikia

Je umejisajili #MwangwiwaUkarimu #EchoesofKindness
#HabarileoUPDATESCC

Habari Zifananazo

Back to top button