CCM yatoa onyo kali

yataka wakwamishaji kuondoshwa

TANGA: Chama Cha mapinduzi (CCM) mkoani Tanga kimesema hakitovumilia watendaji ambao watakuwa sababu ya kukwamisha miradi ya maendeleo na kusababisha wananchi kukosa huduma.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdurahman wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa ilani ya Chama kwa serikali katika kipindi cha mwezi Januari hadi June mwaka 2023.

Amesema kuwa serikali inaleta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ili kusogeza huduma karibu na wananchi lakini watendaji wachache wamekuwa wakitumika kuhujumu miradi hiyo.

“Sisi Chama kwa Mkoa wa Tanga hatutakuwa tayari kuona dhamira nzuri ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kupeleka maendeleo kwa wananchi inakwamishwa na watumishi wachache “amesema

Hata hivyo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Hashim Mgandilwa amesema kuwa katika kipindi cha miezi sita serikali imeweza kutekeleza ilani ya Chama kwa kiwango kikubwa.

“Mkoa umeendelea kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uimarishaji wa mifumo ya biashara na uwekezaji Ili kufungua fursa za kiuchumi mkoani humo”amesema DC Mgandilwa.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button