CDEA kuendesha mafunzo kwa wanamuziki

SHIRIKA la Utamaduni la Maendeleo Afrika Mashariki (CDEA) linaendesha mradi wa mafunzo maalum kwa wanamuziki vijana wanaochipukia wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Uendeshaji huo ni kwa ufadhiri wa Braid Arts & Culture Fund, ambapo vijana hao kujifunza aina mbalimbali za uandishi wa muziki wa jukwaani, na namna ya kulitawala jukwaa (techniques on stage performance).

Meneja mradi wa ubunifu wa CDEA, Angela Kilusungu amesema katika mradi huo unahusisha vijana katinya miaka 18 na 35 utaanza na vijana wakike wawili na wakiume watatu watakuwa katika mafunzo ya miezi mitatu na kazi zao za kimuziki zitasimamiwa na kampuni yao.

Advertisement

Angela amesema katika mafunzo hayo ya miezi mitatu watakuwa chini ya mwanamuziki mkongwe John Kitime ambaye pia wataandaa wimbo wa pamoja na wasanii hao.

Aidha, vijana hawa wataendelea kusimamiwa na CDEA katika shughuli zao kimuziki kwa kutafutiwa nafasi ndani ya Afrika Mashariki kwenye majukwaa ya Sanaa na Utamaduni.

Mradi huo wa uwezeshaji Vijana katika muziki wa moja kwa moja (Live performance) ni wa kwanza kufanyika chini ya CDEA ambapo unatarajiwa kuwa wa manufaa makubwa kwa vijana Tanzania.

2 comments

Comments are closed.