“Chagueni mtu sahihi wakuleta maendeleo”

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Rajab Abdurahman amewataka wananchi wa kata ya Mkuzi kufanya tathimini ya mtu sahihi ambaye ataweza kuleta maendeleo

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo ambapo amesema kuwa kata hiyo ipo nyuma kimaendeleo hivyo wafanye tathimini ya kumpata mwakilishi mzuri wa kuwasemea katika halmashauri.

“Sikilizeni hoja za wagombea wote wanafasi za udiwani kisha msifanye makosa katika uchaguzi huu hakikisheni mnapata Mwakilishi ambaye ataweza kuwasemea na kupigania maendeleo katika kata hii bila ya kusubiri kusukumwa,”amesema.

Naye mgombea wa nafasi ya udiwani kupitia CCM George Chambai amewahakikishia wananchi wa kata hiyo kuwaletea maendeleo endapo watamchagua katika nafasi hiyo ya udiwani.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetanga uchaguzi mdogo wa nafasi za udiwani kwenye maeneo mbalimbali nchini na uchaguzi unatarajiwa kufanya mnamo Machi 20 mwaka huu

Habari Zifananazo

Back to top button