‘Chagueni viongozi wenye hofu ya Mungu’

MTWARA; MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amewaomba viongozi wa dini kuhamasisha waumini kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu na kuchagua viongozi wenye hofu ya Mungu.

Sawala ametoa wito huo, wakati akizungumza na viongozi wa dini mkoani kuhusu masuala ya maendeleo ya mkoa na namna ya kushirikiana kuhakikisha amani, upendo na mshikamano, ili kuuletea mkoa maendeleo.

Isome pia:https://habarileo.co.tz/ulinzi-kuimarishwa-uchaguzi-serikali-za-mitaa/

“Niwaombe sana viongozi wangu, kwenye nyumba zetu za ibada, tusiache kuwakumbusha wananchi wetu kwanza wajue masuala ya uchaguzi ni suala la kikatiba na wao wana haki ya kikatiba kugombea, ili kumpata kiongozi mwenye hofu ya Mungu, tukipata kiongozi mwenye hofu ya Mungu tutapata taifa lililo bora,” amesema.

Amewaomba viongozi hao pia kuwahamasisha wananchi Kwenda kwenye vituo vya kujiandikisha ili kupiga kura ifikapo Novemba mwaka huu kuchagua viongozi wa serikali za mitaa na vijiji.

Isomepia https://habarileo.co.tz/samia-asisitiza-haki-uchaguzi-wa-serikali-za-mitaa/

Pia Sawala amewataka viongozi hao kuhamasisha wananchi kujitokeza kutoa maoni yao kutengeneza dira nyingine ya taifa ya maendeleo ya miaka 25 mingine ijayo kuanzia mwaka 2025 mpaka 2050.

Sawala amewaambia viongozi hao wa dini kuwa kuna timu ya wataalamu itakuja kwenye mkoa kuzungumza na viongozi wa dini pamoja na wananchi ili kupata maoni yao namna wanavyotaka Tanzania iwe kwa miaka 25 ijayo, kuanzia 2025 mpaka 2050 kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi

Habari Zifananazo

Back to top button