Chalamila asema Dar shwari hamna shari

DARES SALAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema Dar es Salaam ni salama tofauti na ilivyoripotiwa na chombo kimoja cha habari

“Tumetoka kwenye Pasaka, kuna gazeti liliandika mauaji yarindima Dar, nikuhakikishie Mheshimiwa Rais hakuna mauaji yaliyorindima mkoani kwetu…tuko salama na kama yatakuja kurindima hao watakaosababisha yatawakuta, ” amesema Chalamila na kuongeza:

“Tunafahamu wakati wa uchaguzi kuna wawekezaji wanaogopa kuweka mitaji yao kwa kuhofia vurugu zinaweza kujitokeza.

Advertisement

“Nichukue fursa hii kuwakaribisha wawekezaji waje hususani katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu…tunathibitisha uchaguzi utakuwa imara, amani na utulivu, hiki ndo kipaumbele chetu,” amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila katika uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ameizindua.