Chalamila atoa ahadi kwa wawekezaji mabenki
DAR ES SALAAM: BENKI ya Maendeleo leo jijini Dar es Salaam imezindua tawi jipya eneo la Mbagala huku ikitambulisha huduma mbili za Nufaika biashara na huduma ya rasimisha ardhi.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema serikali itajenga kituo kikubwa cha polisi Mbagala ili kudhibiti matukio ya kihalifu na kuwataka wawekezaji wa mabenki kuwekeza bila wasiwasi.
Chalamila pia amesema serikali itajenga kituo kikubwa cha biashara inayofanana na Kariakoo ili kurahisisha huduma za biashara kwa mikoa kusini hivyo kuwepo kwa uhitaji wa huduma za kibenki.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizundua tawi la benki ya Maendeleo na kutambulisha huduma mbili za benki hiyo chalamila amesema wanajipanga ili huduma za kibiashara zifanyike kwa saa 24 katika jiji hilo.
Amesema huduma mbili zilizozinduliwa ni nufaika biashara na rasimisha ardhi ambapo benki itatoa mikopo kwa wateja wake.
“Namshukuru mkuu wa kanisa na viongozi wote kwa maoni haya mtu wa kawaida hawezi kuelewa umuhimu wa benki kazi yenu ni kubwa na mnafikia watu wengi hivyo mchango ni mkubwa kwa nchi yetu.
Ameongeza “Jambo kubwa ambalo likinitesa miaka mingi ni usalama na tunashukuru jeshi la polisi na tutafungua kituo kikubwa cha polisi tunaangalia upande huu kwa jicho kubwa hasa wakati huu tunajipanga kufanya biashara kwa saa 24.
Chalamila ameeleza kuwa katika Progaramu hizo mbili ikiwemo rasimisha ardhi benki ilifanya utafiti kuwa wafanyabisha wadogo wanashindwa kuwa na dhamana ya kuchukua mkopo benki kutokana na kutokurasimishwa maeneno6 na hao ndio wateja wao hivyo watawasaidia wengi.
“Kuna mikopo ambayo haina masharti mengi lakini lazima irejeshwe na niwaase vijana wote ambao wanataka kupata mikopo kwasababu ni tiba kiuchumi kama utatambua namna ya kutumia wafike maendeleo benki.
Amewapongeza Maendeleo benki kuanzisha tawi hilo pamoja na kuongeza huduma na kuwataka wateja kutoogopa kutumia mikopo hiyo.
Mkurugenzi wa Maendeleo benki,Dk Ibrahim Mwangalaba amesema tawi hilo limenzishwa kutoa huduma kwa watu wote zikiwemo huduma za mikopo kama kwa wamachinga,mikopo ya vikundi,mikopo ya kuku,mikopo ya nishati jadidifu na mikopo ya nufaika biashara.
“Kuna mikopo ya uboreshaji makazi na huduma zingine kama utunzaji wa amana za wateja,ubadilishaji wa fedha za kigeni ,elimu na ushauri wa biashara na fedha.
Kwa upande wake Msaidizi wa Askofu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dean Lwiza amesema sasa maendeleo benki ina matawi matano na amana ya Sh bilioni 90.7.
“Miaka iliyopita hatukuwa na hizi takwimu inaonesha benki inakua,inaaminika na haijaangalia rangi,kabila na imani za watu inatoa huduma kwa wote.