Chalamila: Changamkie fursa

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka wananchi kuchangamkia fursa, katika mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika(AGRF), unaotarajia kuanza Septemba 5 hadi Septemba 8 mwaka huu

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 3, 2023 Chalamila amesema  mkutano huo utaudhuriwa na washiriki zaidi ya 3000,  hivyo kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo katika ujasiriamali na kuongeza kipato.

“AGRF ni jukwaa kuu la kilimo pamoja na mambo mengine limekuwa likiweka mipango na mikakati ya kiutendaji sambamba na kuhakikisha wanajadili kwa kina kuhusu usalama wa chakula barani Afrika.

Advertisement

“Wananchi wa Dar es Salaam na maeneo mengine mnapaswa kuchangamkia fursa ambazo zitatokana na kufanyika mkutano huu mkubwa.

Kupitia mkutano wa jukwaa hilo pia tutapata fursa za kujifunza teknolojia za kisasa pamoja na na kuongeza uzoefu na hatimaye tutafikia malengo yaliyowekwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Maandalizi yamekamilika,  mkutano huu mkubwa utaleta matokeo chanya katika uendelezwaji wa mifumo ya chakula kwa nchi za Afrika, ukuzaji sekta ya utalii, uwekezaji sekta ya kilimo na biashara.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere JNICC Ephrahim Mafuru amesema kwamba katika kufanikisha mkutano huo Sh.bilioni 12.5 zimetolewa huku akifafanua JNICC wamejipanga vema kuwapokea na kuwahudumia washiriki wote

 

 

5 comments

Comments are closed.