Chalamila: Dar hakuna uhaba wa mafuta

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema mafuta yapo ya kutosha katika mkoa huo.

Chalamila amelazimika kutoa ufafanuzi huo mbele ya Waziri Mkuu na Naibu waziri Mkuu katika Kongamano la Nishati ambalo linafanyika  Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Chalamila kuna minong’ono inayosambaa kuhusu kukosekana kwa Nishati hiyo jijini Dar es Salaam na amewataka watumiaji wa nishati hiyo kupuuza taarifa hizo.

1 comments

Comments are closed.