Chalamila: Msikimbie hoja za CAG

DAR ES SALAAM; MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kinachosabisha Halmashauri kupata hati chafu au hoja kuwa nyingi, inatokana na  baadhi yawatumishi kuikimbia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Chalamila amesema hayo aliposhiriki Baraza la Hoja za CAG Halmashauri ya Ubungo, ambapo kwa miaka mitano mfululizo wamepata hati safi.

” Ofisi ya CAG huwezi kuikimbia. Kwa halmashauri Ofisi ya CAG ni kama mgonjwa na daktari au trafiki na dereva. Ni jambo ambalo ni endelevu mtaishi tu kwa pamoja,” amesema.

Advertisement

Amewataka watumishi kuwatumia vyema wakaguzi wao wa ndani kwa kuwa wanaangalia mambo kwa umakini, kabla ya ofisi ya CAG haijafika kuangalia mambo ya msingi.

Awali Meya wa halmashauri hiyo, Jaffary Nyaigesha amesema kulikuwa na hoja 138, tayari hoja 98 zimefungwa zimebakia 40.