Chalamila: Tulieni barabara zinarekebishwa

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mvua ikiendelea kurekebishwa kuhakikisha miundombinu hiyo inajengwa kwa ubora na uimara.

Chalamila ameyasema hayo leo, Februari 5, 2024, alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa madaraja mawili yaliyovunjika kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha, daraja la Mbezi Msumi linalounganisha Wilaya ya Ubungo na Kinondoni na daraja la Mbopo,  ambapo amesema kuwa zaidi ya madaraja 13 yaliathiriwa na mvua mkoani humo.

Aidha, Chalamila amewataka wananchi waishio mabondeni kuhama mara moja ilikuepuka athari zinazoweza kusababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha na kuwataka wananchi kuacha kufanya shughuli kando kando ya mito jambo linasobabisha kuharibu miundombinu ya barabara.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake mkazi wa mtaa wa Msumi, Erick Lyalya amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kufika eneo hilo kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo kwasasa wametengeneza kivuko cha muda ambacho mwananchi hulipa Sh elfu moja ili kuvushwa.

Aidha wananchi hao wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwa kujibu kwa uharaka pale alipopewa taarifa za kuvunjika kwa daraja hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button