DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila awewaagiza watendaji wote wa serikali zoezi la kufanya usafi ni kwa kila wiki sio kila mwezi kama ilivyokuwa awali ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam, kwenye mkutano na watendaji wa serikali kuhusu tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
Chalamila amesema watendaji hao wahakikishe uchafu unaokusanywa na wananchi usikae kwa muda mrefu katika makazi ya watu na kuwataka waanze mchakato wa haraka wa kubinafsisha dampo la Pugu au waingie hubia na watu wenye nguvu.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Dar es salaam, Mohamed Mang’una amesema mpaka sasa mkoa huo haujaripotiwa ugonjwa wowote wa kipindupindu.
Aidha, Mang’una amesema kuwa wananchi wa Wilaya zote wachukue tahadhari kwa kuyaweka mazingira salama dhidi ya ugonjwa huo wa kipindupindu.
Hata hivyo, Januari 23 na 24, 2024 kutakuwa na zoezi la usafi wilaya zote ambapo zoezi hilo litafanywa na wananchi wakishirikiana na vyombo vya dola