Chalamila: Wafanyabishara zingatieni sheria za kulipa kodi

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewataka wafanyabiashara kuheshimu sheria za ulipaji kodi kwa kutoa risiti na kulipa kodi pindi wanapouza bidhaa zao kwa kutumia mashine za risiti za kielektroniki (EFD).

Pia amewaonya wafanyabiashara kuepuka migomo wakati wanapofanyiwa mabadiliko ya makadirio ambayo hawaridhiki nayo, ni vyema wakafika kwenye Mamlaka husika ili kutatua changamoto zao.

Chalamila amesema hayo leo Septemba 23 ,2023 wakati akizindua wiki ya mashine za risiti za kielektroniki (EFD) kuanzia Septemba 23 hadi 30 mwaka huu , katika viwanja vya Jakaya Kikwete, Dar es Salaam.

“Najua chombo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hakiwezi kupendwa msipoteze muda kwenye kupendwa kwasababu taifa hili linahitaji kodi na kodi ndio mfumo wa taifa letu kwenda mbele, achaneni na migomo. Migomo si afya ni vizuri mkalilia mabadiliko ya sheria na mifumo ya kodi iboreshwe kuliko kuandamana,” amesema Chalamila.

Pia ameitaka TRA iendelee kutoa elimu kwa walipa kodi ili kuepusha migomo isiyokuwa ya lazima.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Fedha wa TRA, Dinah Edward akimwakilisha Kamishna Mkuu, Alphayo Kidata amesema Mkoa wa kikodi wa Ilala ndio unaongoza kwa ukusanyaji wa mapato Tanzania.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x