Chama afungiwa mechi tatu

KIUNGO wa Simba, Clatous Chama amefungiwa michezo mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kutozwa faini ya Sh 500,000.
Uamuzi huo umetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), kutokana na kumkanyaga makusudi mchezaji Abal Kassim wa Ruvu Shooting wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara hivi karibuni, tukio lililotokea wakati wachezaji hao hawagombei mpira.
Kutokana na uamuzi huo, Chama sasa atakosa michezo miwili iliyobaki ya kumaliza msimu, ambayo timu yake itacheza.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
trackback
3 months ago

[…] post Chama afungiwa mechi tatu first appeared on […]

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x