GOLI la mchezaji wa Simba SC, Clatous Chama alilofunga dhidi ya Horoya kwa mpira wa adhabu limeteuliwa kuwa goli bora la wiki kati ya magoli yote yaliyofungwa kwenye mechi za raundi ya tano hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Shirikisho la soka Afrika CAF wametanga kupitia ukurasa wao wa Twitter kuwa nyota huyo raia wa Zambia ameshinda goli bora la wiki.
Chama bado yupo kwenye hatua nzuri ya kushinda mchezaji bora wa wiki ambapo CAF wanawashindanisha wachezaji wanne kwenye kinyang’anyiro hicho. Wanaoshindanishwa ni Sadio Kanuote wa Simba, Mahmoud Kahraba na Percy Tau wa Al-Ahly akiwemo na Chama.
Wiki iliyopita Chama alishinda tuzo ya goli bora na goli lake dhidi ya Vipers liliteuliwa katika kinyang’anyiro hicho.