DAR ES SALAAM: Uongozi wa Klabu ya Simba umetangaza kuwasimamisha wachezaji Nassor Kapama na Clatous Chama kutokana na utovu wa nidhamu.
Taarifa ya iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya Simba Desemba 21, 2023 imeeleza kuwa kufuatia vitendo vya utovu wa nidhamu imepelekea kuchukua maamuzi hayo.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa wachezaji hao watafikishwa kwenye kamati ya nidhamu kwa hatua zaidi.
Uongozi wa Simba umeendelea kuwakumbusha watumishi wote kuzingatia misingi ya maadili na nidhamu kwani klabu haitosita kumchukulia hatua yeyote atakaethibitika kwenda kinyume na utaratibu.
Comments are closed.