Chamwino yatoa hati 11, yapima ekari 6,600

KATIKA kutatua migororo ya wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Chamwino mkoani hapa Halmashauri ya Wilala ya Chamwino imepima zaidi ya ekari 6,600 kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi kwa wakulima na wafugaji katika wilaya hiyo. Katika upimaji huo, pia hati 11 kati ya 20 zilikabidhiwa kwa walengwa ambao ni wakulima na wafugaji.
Pia, katika hilo waliwatambua wakulima 87 na mashamba 1,317 ya wakulima katika maeneo hayo. Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Dodoma, Rosemary Senyamule katika Kijiji cha Fufu wilayani Chamwino, Ofisa Maendeleo ya Ardhi katika Wilaya ya Chamwino, Enock Mligo alisema maeneo hayo yalipimwa ili kuondoa migogoro hiyo katika tarafa za Makang’wa na Itiso ambazo migogoro ya ardhi ilikuwa imekithiri.
Akitoa taarifa ya upimaji mipaka na kutolewa kwa hati hizo, Mligo aliyataja maeneo yaliyopimwa ni tarafa za Makang’wa na Itiso ambazo zina wafugaji wengi na migogoro imekithiri. Pamoja na upimaji huo, wafugaji hao pia walitakiwa kufuata masharti ya umiliki ardhi ikiwa ni pamoja na kutunza alama za mipaka na kutunza mazingira.
Akizungumza katika halfa hiyo, Senyamule alisema halmashauri za mkoa huo zinatakiwa kuwasiliana na wizara ya kilimo kwa lengo la kuwatafutia fursa wafugaji walioitikia mwito wa kupima maeneo yao kwa hiari na kufanikisha kupatiwa hati miliki za ardhi na mashamba. SOMA: Mashamba pori chanzo migogoro ya ardhi Kakonko
“Wafugaji wamekubali kufuga ndani ya maeneo yao. Serikali lazima tuwaunge mkono ili waone matunda ya dhamira yao,” alisema. Aliongeza: “Wakurugenzi, muwasiliane na Wizara ya Kilimo ili wafugaji hawa wapate fursa ya kuchimbiwa visima, wafundishwe upandaji wa majani ya chakula na wapate mbegu za kisasa za mifugo”.




TUMA SALAMU KWA BIBI – NJUKA
TUMA SALAMU KWA BIBI – NJUKA