Chana ateua msajili vyama vya michezo
WAZIRI wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Pindi Chana amemteua Evordy Kyando kuwa kaimu msajili wa vyama vya michezo nchini akichukua nafasi ya Riziki Majala.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya serikali Eleuteri Mangi siku ya leo, Juni 19, 2023 lengo la mabadiliko hayo ni kuboresha utendaji kazi wa sekta ya michezo nchini.
Kabla ya uteuzi huo, Kyando alikuwa Kaimu Mkuu wa kitengo cha sheria katika wizara hiyo.
Aidha, uteuzi huo unaanza mara moja.