Chana mgeni rasmi mashindano ya’Lugalo Ladies Open’

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Pindi Chana, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Shindano la “Lugalo Ladies Open 2023”litakalofanyika Mei 20 na 21 Lugalo Gofu Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)amesema ,shindano hilo litashirikisha wachezaji wa klabu za gofu Tanzania nzima hasa Wanawake,ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Pindi Chana.

Naye Hawa Wanyeche Nahodha wa Klabu hiyo kwa Upande wa Wanawake amesema, Shindano hilo linafanyika kwa mara ya tatu mfululizo na mwaka huu litatumika kupata wachezaji watakao iwakilisha Tanzania katika Mashindano ya “East and Central Challenge Trophy”ambalo linalotarajiwa kufanyika Rwanda Novemba 11 mwaka huu.

Advertisement

Kauthari D’Souza Meneja Masoko wa Benki ya Exim ambao ni Wadhamini Wakuu wa Shindano hilo amesema, Mwanamke anamchango Mkubwa katika Michezo na wao wanafuraha kuwa sehemu ya Shindano hilo,na wanawaomba Watanzania hasa Wanawake wajitokeze kwa wingi kushiriki shindano hilo.

Shindano hilo la “Lugalo Ladies Open 2023” Litafanyika Mei 20 na 21 katika Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Lugalo,ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Pindi Chana,huku wachezaji kutoka klabu mbalimbali za Gofu zitashriki ikiwemo Dar Gymkhana,Arusha Gymkhana pamoja na TPC Moshi Golf Klabu.

1 comments

Comments are closed.