Kongamano la ukuaji uchumi kwa njia za asili kufanyika Dar

Upandaji miti unasaidia kupunguza hewa ukaa

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa iliyopo katika biashara ya hewa ukaa.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Mwendeshaji Mkuu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya ADAP, Yves Huasser alipokuwa akizungumzia kuhusu kongamano kubwa linalotarajiwa kufanyika Dar es Salaam, Novemba 16, 2023 kwenye Hotel ya Hyatt Regency.

Amesema kama wananchi wakichangamkia biashara ya hewa ukaa wanaweza kupata fedha za kulipia hata bima ya afya na hilo litawafanya waithamini misitu na kuilinda, hawatakata miti hovyo.

Advertisement

“Ni biashara nzuri ambayo inaweza kuwasaidia wananchi katika maeneo mbalimbali vijijini, lakini pia inasaidia kuboresha mazingira ambayo yanaharibiwa na mabadiliko ya tabianchi, pamoja na baadhi ya shughuli za binadamu,” amesema Huasser.

Amesema kongamano hilo litashirikisha wadau kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Marekani na Ulaya na kwamba utakuwa mkutano mkubwa wa aina yake wenye lengo la kuwajengea uwezo pia wadau kuhusu biasshara ya hewa ukaa.

Ameishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa namna wanavyoshirikiana nao katika masuala mbalimbali kuhusu mambo ya hewa ukaa.

Naye Meneja Uendeshaji wa taasisi ya Africa Carbon Agency, Cosmas Tungaraza amesema kupitia kongamano hilo masuala mbalimbali yatazungumzwa na wadau wataelewa kwa undani zaidi kuhusu biashara ya hewa ukaa.

“Hili ni kongamano la kimataifa linalohusu ukuaji wa uchumi kwa kutumia njia za asili litafanyika tarehe 16 Novemba, 2023, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 12 jioni katika hoteli ya Hyatt Regency iliyopo Dar es Salaam, Tanzania.

“Kongamano limeandaliwa na kamati inayoshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Africa Carbon Agency, ADAP, Carbon Tanzania, na AxessImpact. Kongamano linafanyika kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Nchi (Muungano na Mazingira) – Ofisi ya Makamu wa Rais, pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.

“Karibu ujumuike na  wadau wa sekta ya Kaboni kutoka Tanzania na nje ya nchi kujadili mada mbalimbali zinazohusu sekta hii kwa maendeleo endelevu,” amesema Tungaraza.

 

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *