MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewataka wajasiriamali waliopo katika makundi maalum jijini Dodoma kuchangamkia fursa za zabuni mbalimbali zinazotangazwa na serikali na kwa kuwa sheria ya manunuzi ya umma imeweka bayana fursa hiyo.
Mavunde ameyasema hayo akifungua mafunzo ya uchakataji na usindikaji wa bidhaa chini ya mwavuli wa Wanawake na uchumi wa viwanda, yaliyofanyika Sido – Kizota mjini Dodoma
Amesema, wanayopata wanawake hao yatachochea uongezaji wa thamani wa bidhaa zao na upatikanaji wa soko la uhakika.
“Tunao wajibu wa kuhakikisha mnapata mafunzo stahiki na kupata mitaji ya uhakika itakayowasaidia kuzifikia fursa mbalimbali hasa za serikalini.”
Kifungu cha 64(2)(c) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma 2011 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 ukisoma sambamba na Kanuni Na. 30C ya Tangazo la Serikali Na. 446/2013 linazitaka Taasisi zote nunuzi za serikali kutenga asilimia 30 ya manunuzi yake kwa mwaka kwa ajili ya wakina mama,vijana na watu wenye ulemavu hivyo ni lazima tuhakikishe hizi fursa hazitupiti na tunakuwa sehemu ya manunuzi haya ya umma.”Amesema
Naye Mwenyekiti wa WAUVI Rehema Mbeleke, amesema mafunzo hayo yanayoratibiwa na SIDO yana lengo la kumjengea uwezo mjasiriamali wa Dodoma kulifikia soko kwa urahisi na akachukua nafasi hiyo kumshukuru Mavunde kwa kuwachangia sh milioni 1, ya vifaa vya kufundishia pamoja na kuwanunulia printer ya ofisi kwa ajili ya uratibu wa kazi za kila siku za WAUVI.