Chanjo saratani mlango wa kizazi yafanikiwa 95%
DAR ES SALAAM: WIZARA ya Afya imesema utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa Kizazi umefanikiwa na kufikia asilimia 95 tangu kuanza kutolewa chanjo hiyo Aprili 22, 2024 kwa dozi moja.
Akizungumza wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari ,Meneja wa Mpango wa Chanjo wa Taifa ,Dk Florian Tinuga amesema siku ya kwanza walichanja asilimia 27 huku lengo ni kila siku kutoa asilimia 20.
“Maamuzi ya kufanya mabadiliko ya kutoa dozi moja ni sahihi tunawafikia watoto wengi zaidi ili kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi na utafiti kuonesha kuwa dozi moja inakinga sawa na dozi mbili.
Amesema saratani ya mlango wa kizazi inasababishwa na kirusi cha Papiloma na inaambukizwa kwa njia ya kujamiiana huku dalili zikiwa ni kutoka uchafu au damu ukeni,kupata hedhi bila mpangilio maalum.,
“Mikoa ya Kilimanjaro, Dar es Salaam na Mwanza inaongoza kwa saratani hiyo.
Dk Tinuga amesema mabinti milioni tano watapewa chanjo hiyo ambapo bara ni milioni 4.8 huku visiwani ikiwa ni 187,059 katika mikoa 31.
“Chanjo ni salama na hutolewa bure kwa walengwa kwa hiari na chanjo hiyo hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya mlango wa kizazi inapatikana katika vituo vya kutolea huduma za chanjo na hutolewa vituoni ,kwenye jamii na shuleni na hutolewa wakati wa kampeni na kawaida,”amesisitiza Dk Tinuga.