Njia mbili zinavyosaidia watoto kufikiwa chanjo

SERIKALI imetumia njia ya chanjo mkoba ‘Outreach’ na chanjo tembezi ‘Mobile clinic’   kuwafikia watoto wote chini ya miaka mitano kupata chanjo na kuwakinga  na maradhi mbalimbali.

Outreach ni pale watoa huduma wanatoka na kwenda kuwafikia walengwa umbali wa kilomita tatu au tano na Mobile ‘clinic’ imekuwa ikisaidia wazazi ambao hawawezi kufikiwa na huduma hiyo kwa umbali wa kilomita 20 au zaidi.

Dira ya Maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 inafikiwa kwa malengo yake ya kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano hapa nchini.

Advertisement

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Igalula kata ya Ukune Halmashauri ya Ushetu  wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Helena Cosmas na Lucy Benjamini wanasema wataalamu wa afya wamekuwa wakifika kijijini hapo nakutoa huduma ya chanjo kwa watoto.

Cosmas anasema wamefurahia kupata huduma ya chanjo kwa watoto  kwa ukarbu kwani  walikuwa wanashindwa kwenda umbali wa kilomita 15 kufuata huduma ya kliniki na chanjo  kwa watoto.

“Kutokana na umbali tukishamaliza kujifungua haturudi tena labda mtoto augue lakini akiwa mzima hatuendi sababu ya umbali mrefu  kituo cha afya kipo kijiji  cha Iboja umbali wa kilomita 15 na kwenda  kijiji cha chona umbali wa kilomita 8 “anasema Cosmas.

Benjamini anasema kijiji hakina zahanati utolewaji wa huduma za  kliniki na chanjo kwa watoto hutangaziwa kwenye mkutano wa hadhara kuwa wataalamu watakuwepo na wao hujitokeza.

“Wataalamu wametusaidia  kutotembea umbali mrefu kwani wao wamekuwa wakituletea huduma ya kliniki na kuwapa chanjo watoto wetu kwa  hilo tunaipongeza serikali” anasema Benjamini.

Mtendaji wa kijiji cha Igalula Alex Kabakina anasema kijiji kina wakazi 8000  ambapo wazazi hutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya na kliniki kwa watoto ikiwa wataalamu wamekuwa  wakija kutoa chanjo.

“Lakini zipo jitihada zilizofanyika za ujenzi wa Zahanti ambao ulianza mwaka 2016 kwa nguvu za wananchi  kuchangia  na halmashauri mapato ya ndani ikatoa  Sh millioni 14 na Serikali Kuu ilitoa Sh milioni 50 mpaka kukamilisha.

”anasema Kabakina.

Diwani wa kata ya Ukune, Mkomba Paul anasema kata yake ina wakazi zaidi 1500 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi na vijiji nane  ambavyo ni  Iboja,kundikili, Igalula, Chibisa, Sofi Ilwilo, Italike na Kayenze lakini  kijiji kimoja ndiyo kina kituo cha afya pekee.

“Tumeanzisha ujenzi wa Zahanati hii baada ya kuona  wajawazito wanateseka kutembea umbali wa kilomita 15 kwenda kituo cha afya Ukune kilichopo kijiji cha Iboja  na wakati mwingine  kwenda zahanati iliyopo kata ya Mapamba ni mwendo wa kilomita 10 au Chona kilomita nane. ”anasema  Paul.

Diwani Paul anasema kukosekana kwa zahanati katika vijiji vya kwenye kata yake wataalamu wa afya wamekuwa wakijitahidi kuwafikia wananchi walipo na kuwapa huduma ya kliniki watoto na chanjo.

Mbunge wa jimbo la Ushetu Emanuel Cherehani anasema yalikuwepo maboma ya zahanati 23 yaliyoanzishwa mwaka 2016 lakini kipindi cha miaka miwili maboma 14 ya zahanati yamekamilika na zahanati 11 zinawatumishi zimeanza kutoa huduma.

“Sera ya afya ya mwaka 2007 inaeleza kila kata kuwe na kituo cha afya na kila kijiji kuwe na zahanti  na serikali inafanya jitihada  za kuhakikisha sera hiyo inatekelezwa ipasavyo na wananchi wasitembee umbali mrefu kufuata huduma. ”anasema Cherehani.

Mratibu wa huduma za afya, Musa Baraza anasema kuna  hospitali moja, vituo vya afya  vitatu na zahanati 31 na  vituo hivyo vina huduma za palepale na  huduma za kuwafikia walengwa waliopo mbali.

Baraza anasema halmashauri ina  jumla ya huduma za mikoba (Outreach) kila mwezi huduma ya chanjo zinafanywa 81 na Mobile Clinic nne na robo ya mwaka huu huduma zilizofanywa za Outreach 243 na Mobile Clinic 12.

“Katika robo ya pili mwezi Juni wamefanya Outreach  238  na Mobile kliniki 12 na Malengo wamefikia asilimia 99 kwa watoto  waliowafikia  mfano chanjo ya kuzuia kuhara Rotavaccine  mwezi  AprilI walitoa  Dozi ya kwanza ya Rota  nakufikiwa watoto 816, Mei watoto  829 na Juni watoto  775”anasema Baraza.

Baraza anasema wahuduma ngazi ya jamii (WAJA) wako 554  ambao wamekuwa wakihamasisha  jamii na kila kitongoji wapo  na lengo lililopo  kuwafikia watoto na wajawazito.

Mratibu wa chanjo wa Halmashauri ya Ushetu, Saulo Mkama anasema wamekuwa wakitoa huduma za chanjo Outreach imekuwa ikiwasaidia wananchi  kutotembea umbali mrefu.

“Outreach ni pale watoa huduma wanatoka na kwenda kuwafikia walengwa umbali wa kilomita tatu au tano  na Moble kliniki imekuwa  ikisaidia wazazi  ambao hawawezi kufikiwa  na huduma hiyo kwa umbali wa kilomita 20 au zaidi”.

Mganga Mkuu wa Halmashauri Ushetu, Dk Athumani Matindo anasema kuna  vijiji 112 kati ya hivyo vijiji 35 ndiyo vimefikiwa na  huduma ya  kutolea afya na vijiji vingine havina  lakini wataalamu wamekuwa wakienda kutoa elimu ya afya, kliniki na chanjo.

“Tumekuwa tukishirikiana  na viongozi wa kijiji kupata maeneo ya kutolea huduma wakati wataalamu wakifika  ikiwa huduma wanazo zikosa ni zile na mama na mtoto lazima waende kwenye kituo cha afya kwenye  vifaa”anasema dk Matindo..

Mratibu wa chanjo mkoa Timothy Sosoma anasema  Outreach imesaidia   kuwafikia watoto wengi walio na umri  chini ya miaka mitano kupata chanzo za aina zote zinazohitajika  hadi kufikia mwezi June  mwaka huu watoto 39512  wameapata chanjo ya Rota  sawa na asilimia 109.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Nuru Mpuya anasema kuna vituo 307 vya kutolea huduma za afya na watoto wamekuwa wakipata chanjo za aina zote pale wanapohitajika wengine kupitia Outreach na Mobile Kliniki.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu anasema huduma ya Outreach na Mobile imechangia kupunguza vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa kufikiwa na huduma ya chanjo maeneo  walipo.

4 comments

Comments are closed.