Chanzo umeme kukatika usiku wa manane

DODOMA: SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kutokea hitilafu kwenye mfumo wa njia ya kusafirishia umeme kwenye Gridi ya Taifa, hali iliyofanya maeneo mbalimbali nchini kukosa umeme.

Taarifa iliyotolewa usiku wa manane ya leo Aprili Mosi, 2024 na Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TANESCO Makao Makuu-Dodoma, inaeleza kuwa wataalamu kutoka shirika hilo wanaendelea kufanya marekebisho ili huduma zirejee haraka iwezekanavyo.

“Shirika linawaomba uvumulivu wateja wake katika kipindi hichi ambacho huduma ya umeme inakosekana,” imeeleza taarifa hiyo ya TANESCO.

Habari Zifananazo

Back to top button