Chanzo vifo watu 11 Mtibwa chatajwa

WATAALAMU 11 wa umeme na mitambo wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa mkoani Morogoro wamekufa na wawili wamejeruhiwa.

Watu hao walipoteza maisha usiku wa kuamkia jana baada ya bomba linalosafirisha mfumo wa mvuke kupasuka katika maungio kwenye mfumo mpya uliosimikwa kwenda kwenye chumba cha nishati ya kuzalishia umeme.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Shaban Marugujo alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea saa 7:30 usiku katika kiwanda hicho kilichopo Turiani wilayani Mvomero.

“Boila namba nne ambalo linapitisha presha ya mvuke ambayo inatoka kwa ajili ya kuingia kwenye tabani katika chumba cha Power House ambayo inazalisha umeme na hiyo haiwezi kufanya kazi bila msukumo kutoka kwenye boila namba nne,” alisema Marugujo.

Marugujo alisema kwenye maungio paliachia huo mvuke kwa nguvu na kwamba bomba hilo uwezo wake ni kubeba bar 45 liweze kuhimili kubeba mzigo kwenda kwenye tabani.

“Inavyoonekana katika yale maungio haukuweza kuhimili na kuweza kuachia na huo msukumo ilipotoka ikaweza kwenda kupika katika hiki kibanda ambacho ni cha uongozaji ambapo kuna wataalamu mbalimbali wanaoendesha panel na kusimamia hiyo turban,” alisema Marugujo.

Alisema ajali hiyo pia imesababisha hitilafu ya uharibifu wa mali kwa maana ya mtambo husika, taharuki kwa wananchi wengine na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama alisema miongoni mwa waliokufa kuna raia watatu wa kigeni kutoka Kenya, India na Brazil na waliobaki ni Watanzania.

Kamanda Mkama alisema miili ya watu hao ilihifadhiwa katika chumba ya maiti cha hospitali ya kiwanda cha sukari Mtibwa. Mganga Mfadhiwi wa Hospitali ya Turiani, wilayani Mvomero, Dk David Ruchwanisa alisema saa kumi usiku walipokea majeruhi wawili wanaume wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 28 hadi 32 na walipata huduma ya kwanza na kupewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Benjamin
Mkapa, Dodoma.

“Majeruhi hawa wamepata majeraha sehemu za uso, kifuani, tumboni, miguu pamoja na mikono na hali zao si nzuri sana na tunatarajia baada ya kupata huduma na matibabu zaidi watapona,” alisema Dk Ruchwanisa.

Mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi wa kiwanda hicho, Nicolaus Ngowi alisema tukio hilo linahuzunisha sana. Ngowi alitoa pole kwa wafanyakazi na wanachama wote wa TPAWU, viongozi na kampuni kwa ujumla.

Alisema wanaomba taasisi zinazohusika na masuala ya wafanyakazi na usalama mahala pa kazi zifanye uchunguzi kufahamu nini kilisababisha madhara hayo.

Alihimiza tahadhari zichukuliwe kwenye mazingira ya kazi ili wafanyakazi wawe salama sehemu za kazi hasa usiku. Ngowi pia aliuomba Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ufike kiwandani hapo na kufanya ukaguzi kuhakikisha wafanyakazi wote waliopata madhara na familia zao zinafidiwa.

“Jamii imepoteza ndugu zao ambao walikuwa ni tegemeo katika familia zao na sasa ndoto zao zimekatizwa …tunaomba mfuko huu uweze kushughulikia kwa utaratibu unaopaswa,” alisema. Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji walifika kiwandani hapo kutoa pole wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Mali

Habari Zifananazo

Back to top button