Chapa ya Guinness kudhamini EPL

Dar es Salaam: Guinness imesaini mkataba wa miaka minne unaoiwezesha chapa hiyo kuwa miongoni mwa wadhamini wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Ikijivunia nafasi yake kama mshirika rasmi wa unywaji makini katika ligi, Guinness inatarajia kutumia ushawishi wake wa kimataifa kukuza na kudumisha viwango vya unywaji kwa uwajibikaji katika kipindi chote cha msimu.

Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL), ambayo inauza Guinness nchini Tanzania, itatumia uzoefu wake katika masoko, matangazo ya ubunifu, na historia yake ya kuwezesha udhamini wa michezo yenye viwango vya ubora wa hali ya juu duniani kujenga uzoefu wa kipekee na kufurahisha mashabiki.

Advertisement

Ushirikiano huu utalenga kusaidia na kuinua jamii ya mpira wa miguu, uwanjani na nje ya uwanja, na kuchochea uhusiano mpya kati ya wateja wake na mashabiki na wapenzi wa Ligi Kuu ya England kote ulimwenguni.

Wankyo Marando, Meneja wa Chapa ya Guinness wa SBL, alisema: “Ushirikiano huu unatangaza zama mpya za kusisimua kwa Guinness nchini Tanzania.

“Kwa kushirikiana na EPL, sio tu tunainua chapa yetu lakini pia tunawasogeza karibu wateja wa Tanzania
na ligi maarufu zaidi ya mpira wa miguu duniani. Ni muunganiko kamili wa shauku ya
mpira wa miguu na upendo kwa bia bora, ambao tunaamini utawagusa kiundani wateja
wetu.”