RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amemteua Charles Hilary kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali visiwani humo.
Awali kabla ya uteuzi huo, Hilary alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu, Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Februari 6, 2023 na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imesema uteuzi umeanza leo.
Hata hivyo, cheo hicho hakijawahi kuwepo ndani ya serikali ya awamu zote za Zanzibar.