Chato festival kufanyika Novemba 26 Chato

TAMASHA la Utalii la Chato Festival limepangwa kufanyika Novemba 26 hadi Desemba 3, mkoani Chato.

Akizungumza leo Oktoba 4, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Deusdedith Katwale amesema lengo la tamasha hilo ambalo litafanyika na maonesho ya bidhaa mbali mbali, lina lengo la kukusanya fedha ambazo zitasaidia ujenzi wa madawati 29,000 kwa shule za msingi.

Amesema pia, lengo ni kutangaza utalii katika ukanda wa Chato ili kukuza sekta ya utalii nchini.
“Mpaka kufika 2025 Chato tunatarajia kuwa na watalii wasiopungua milioni tano, na Utalii Festival ni moja ya mkakati wetu kufikisha idadi hiyo.” Amesema Katwale.

Amesema tamasha hilo litafungua fursa mbali mblai za wafanyabiashara kutangaza bidhaa zao katika maonesho yatakayofanyika katika tamasha hilo ambalo pia litapambwa na mechi ya mashabiki wa Simba na Yanga.
“Tuna upungufu wa madarasa 29,000 chochote kitakachopatikana katika tamasha la Chato Festival kitaelekezwa kwenye ununuzi wa madawati,”amesema.

Nae, Muhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Rubondo, Dk Imani Kikoti amesema washiriki wa tamasha hilo watapata fursa ya kuona maji ya blue ndani ya kisiwa cha kijani.

Pia, wataona swala wakubwa ambao wanapatikana hifadhi ya Rubondo tu na aina 400 za ndege.
“Kuna eneo la maji matakatifu, miaka ya nyuma kabila la Wazinza walikuwa wanatumia kutambika mfano mtu anasumbuliwa na uzazi hapati mtoto basi walitumia maji hayo, pia yalitumika kuondoa mikosi, ndio maana yakaitwa maji matakatifu.”Amesema Dk Kikoti.

Kwa upande wa Afisa Muhifadhi Mkuu Burigi Chato, Ismaily Omari amesema hifadhi hiyo yenye kilomita 4, 707 ni ya nne kwa ukubwa licha ya uchanga wake mpaka sasa inawageni 78 wa nje na 575 watanzania idadi ambayo amekiri kuwa bado ni ndogo. Hifadhi hiyo ilianzishwa rasmi 2019.

Amesema lengo ni kufikia idadi ya wageni 1,000 watanzania na 500 wa nje hadi kufikia 2025.
Aidha, amesema washiriki wa Tamasha la Chato Festival watajionea aina zaidi ya 41 za Wanyama na 400 za ndege wakiwemo wenye midomo kama kiatu wanaovua Samaki na kuwala.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button