‘ChaWote’ kuwajaza wateja mapesa

Kampuni ya huduma za mawasiliano Tigo imezindua kampeni mpya inayojulikana kama ‘ChaWote’ itakayowawezesha watumiaji wa mtandao huo kujishidia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu Shilingi 5,000,000.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Angelica Pesha amesema promosheni ya kipekee kwani kila mteja wa kampuni hiyo ni mshindi.

“Kampeni hii inawapa wateja nafasi ya kujishindia zawadi za fedha taslimu hadi Sh 5, 000, 0000 na bonasi za papo hapo za hadi dakika 100 na SMS 100 kwa siku 90, Ili kuweza kuwa mshindi kwenye kampeni hii ya ChaWote, wateja wa Tigo wajinunulie vifurushi vyao pendwa vya siku,” amesema.

“Ili kunufaika na mpango huo, ameongeza, mteja huyo huduma au bidhaa kupitia Lipa kwa Simu watapa bonus za papo hapo za dakika na SMS na kuingia kwenye droo inayowapa nafasi ya kujishindia hadi TSh 1,000,000 kila siku na TSh 5,000,000 kila mwezi,” ameongeza.

 

Habari Zifananazo

Back to top button