Chelsea hii sasa sifa

CHELSEA imekamilishauhamisho wa mkopo wa miezi sita wa mchezaji Joao Felix kutoka Atletico Madrid mpaka mwisho wa msimu huu.

“Chelsea ni miongoni mwa timu kubwa duniani, matumaini yangu nitaisaidia kufikia malengo ya timu, nina furaha sasa kuwa hapa na kucheza Stanford Bridge.” amesema Felix.

Kabla ya kwenda Chelsea, Felix alishasaini mkataba mpya na Atletico ambao utakamilika mwaka 2027, hivyo baada ya msimu kuisha atarejea Atletico kuendelea na kukipiga na timu hiyo.

Advertisement