CHELSEA inaendelea kupangua kikosi chao baada ya taarifa kuwa kiungo Hakim Ziyech anakaribia kujiunga na Al Nassr ya Saudia Arabia anayochezea Cristiano Ronaldo.
Taarifa zinaeleza makubaliano binafsi kati ya Ziyech na Al Nassr yameafikiwa kama mipango ikienda ilivyopangwa Ziyech atasaini mkataba wa miaka mitatu hadi Juni 2026.
Taarifa ya Fabrizio Romano imesema Chelsea pia wamekubali kumuuza mchezaji huyo kwenda Uarabuni.
24 Feb 2020 Ziyech alijiunga na Chelsea akitokea Ajax ya Uholanzi na kusaini mkataba wa miaka mitano hivyo hadi sasa imebaki miaka miwili.
Comments are closed.